The Guardian, TMF kuwanoa waandishi viwango habari za tija

By Christina Mwakangale , Nipashe
Published at 04:43 PM Nov 11 2024
Dastan Kamanzi Mkurugenzi Mtendaji wa TMF akielezea muundo wa dawati la Tija (Tija Desk) lililozinduliwa leo.
Picha:Mpigapicha Wetu
Dastan Kamanzi Mkurugenzi Mtendaji wa TMF akielezea muundo wa dawati la Tija (Tija Desk) lililozinduliwa leo.

KAMPUNI ya The Guardian imeweka makubaliano na Tanzania Media Foundation (TMF), kutekeleza mradi wa mafunzo kwa waandishi wa habari za tija.

Habari hizo ni za uchunguzi ambazo zinalenga kuleta mabadiliko chanya kwa umma na kuongeza uwajibikaji, kama vile sekta ya afya, elimu na jamii.

Akizindua programu hiyo leo katika ofisi za kampuni hiyo, Mikocheni, Dar es Salaam, inayotarajia kuanza Jumatatu ijayo, Naibu Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Jackson Paulo, amesema kwamba mradi huo utaleta matokeo chanya kwa kampuni hasa eneo la uchumi.

Pia amesema habari hizo zitakuwa na mafanikio kwa jamii, hivyo watakaonufaika na mradi huo, wawe makini katika kujifunza na kuandika habari za aina hiyo.

Mkurugenzi wa TMF, Dastan Kamanzi, amesema mradi huo wa kipindi cha mwaka mmoja utaleta mabadiliko kwa waandishi wa habari, kwa kuwa yatawasidia kuwajengea uwezo, kuandaa mpango kazi, kufanya utafiti na uchunguzi kabla ya kwenda eneo la kazi, kisha kuandika habari itakayoleta tija kwa umma.