JESHI la Polisi linachunguza picha mjongeo inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha watu ambao wanajaribu kumkamata na kumwingiza kwa nguvu ndani ya gari, Deogratius Tarimo, ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa Kibaha mkoa wa Pwani.
Msemaji wa Jeshi la Polisi Dodoma, Tanzania, DCP David Misime, amesema leo kwamba, ukio hilo liliripotiwa na yeye mwenyewe katika kituo cha Polisi Gogoni, jijini Dar es Salaam Novemba 11, mwaka huu.
Kwanmujibu wa ushahidi uliowasilishwa kituoni hapo na yeye mwenyewe ni kwamba, chanzo cha tukio na kilicho msukuma kufika katika Hoteli ya Rovenpic iliyopo eneo la Kiluvya jijini humo ni kufanya mazungumzo ya biashara ambayo amekuwa akiwasiliana kuifanya na aliokuwa anawasiliana nao tangu Oktoba 25, 2024.
Jeshi la Polisi, lilise.a linahakikisha litawakamata watu waliokuwa wakijaribu kumkamata na kujaribu kumwingiza kwenye gari kama inavyoonekana katika picha mjongeo huo kulingana na ushahidi ambao umeshakusanywa na unaoendelea kukusanywa ili hatua zingine ziweze kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria kwani hakuna aliye juu ya sheria.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED