Polisi yamdaka aliyetishia watu silaha, kujeruhi

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 12:29 PM Oct 28 2024
Kamanda Jeshi la Polisi Kanda Maalum SACP Jumanne Muliro.
Picha:Mtandao
Kamanda Jeshi la Polisi Kanda Maalum SACP Jumanne Muliro.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limekamata Derick Derick Junior, mwenye umri wa miaka 36, mkazi wa Salasala, Kinondoni, kwa tuhuma za kujeruhi na kutishia watu kwa silaha.

Tukio hilo lililotokea saa 12:30 asubuhi katika maeneo ya ‘1245 Night Club’ Masaki, linadaiwa kuhusisha Derick kumjeruhi Julian Bujuru kwa kutumia kitako cha bastola, na kumjeruhi sehemu ya jicho na pua. Mtu huyo aliyejeruhiwa anaendelea vizuri na matibabu.

 Polisi imesema wanakamilisha taratibu za kisheria kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ili mtuhumiwa aweze kufikishwa katika vyombo vya sheria haraka iwezekanavyo.

Hata hivyo  Polisi imetoa wito kwa wananchi kuhusu umiliki wa silaha, likidai kuwa litachukua hatua kali dhidi ya mtu yeyote anayemiliki silaha na kufanya matendo kinyume na sheria.

1