Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Visiwani Zanzibar, Salum Mwalimu amesema wananchi wanaweza kupata maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi katika maeneo yao, iwapo watachagua viongozi waadilifu, watenda haki na wenye maono.
Amesema hayo leo wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya Kapripointi mjini Mpanda mkoani Katavi, ikiwa ni siku za mwisho za kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa zinazotarajia kufanyika kesho nchini kote.
"Viongozi wenye sifa hizo za kuwa na maono ya kiuongozi, uadilifu na watenda haki wapo CHADEMA hivyo wananchi wanapaswa kuwachagua viongozi hao ili waweze kuwaletea maendeleo endelevu kwenye maeneo yao" amesisitiza Mwalimu.
Awali, Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa Katavi, Rhoda Nkuchela amesema pamoja na kufanyiwa figisu katika mchakato mzima wa uchaguzi ikiwemo baadhi ya wagombea wao kuenguliwa njia pekee ya wananchi kuiadhibu CCM ni kupitia sanduku la kura.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED