NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara John Mongella, amehitimisha kampeni za kuwanadi wagombea wa CCM mkoani Shinyanga, ambao watapeperusha bendera ya chama hicho kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, utafanyika kesho Novemba 27 kwa wananchi kupiga kura ya kuchagua Wenyeviti wa Vijiji Mitaa, Vitongoji,pamoja na wajumbe.
Mongella amehitimisha kampeni hizo leo Novemba 26 katika Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga, na kuwanadi wagombea wa CCM kwa wananchi, kwamba kesho wakawapigie kura ili wapate kushinda na kuwaletea maendeleo.
“Kuwachagua Wagombea wa CCM ni kuchagua Maendeleo,Amani na Umoja, na Maendeleo ya Taifa letu yana anzia kwa viongozi wa serikali za mitaa,”amesema Mongella.
Aidha, amesema katika uchaguzi huo wa serikali za mitaa, tayari Wagombea wa CCM katika Mitaa 90, Minne amepita bila ya kupingwa, na Kati ya Vitongoji 2,703 , Vitongoji 2,176 wamepita bila ya kupingwa, huku Vijiji 506,vijiji 307 wamepita bila ya kupingwa, na kuwasihi wananchi wajitokeze pia kuwapigia kura za ndiyo.
Nao baadhi ya viongozi mbalimbali wa Chama hicho wakiwamo Madiwani na Wabunge, wamewaomba wananchi wa Shinyanga, kwamba wakawachague wogombea wote wa CCM ili kuwepo na muunganiko wa uongozi na kuwaletea maendeleo.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED