Takribani 300 wachunguzwa macho

By Christina Mwakangale , Nipashe
Published at 01:56 PM Nov 26 2024
Wataalamu wa afya wakimhudumia mmoja wa waliofika kufanyiwa uchunguzi.
Picha: MNH
Wataalamu wa afya wakimhudumia mmoja wa waliofika kufanyiwa uchunguzi.

MAMIA ya wakazi wa Mbagala, Temeke, Dar es Slaam, wamejitokeza katika Hospitali ya Mbagala Rangi Tatu, kufanyiwa uchunguzi wa macho.

Uchunguzi huo umefanywa na madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), kwa kushirikiana na wenzao hospitalini hapo.

Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke, Dk. Jonas Lulandala, aliwataka wananchi kuendela kujitokeza na kutumia fursa hiyo ya upimaji macho bila malipo, inayoratibiwa na Manispaa ya Temeke kwa kushirikiana na MNH.

Alisema kwamba watakaogundulika na changamoto kubwa zinazohitaji upasuaji, watapata huduma hiyo kupitia upasuaji wa tundu dogo utakaofanyika MNH.

Pia, Dk. Lulandala ameushukuru Uongozi wa MNH na watoa huduma kutoka hospitalini hapo, kwenda kutoa huduma katika maeneo waliko wananchi huku wananchi 300 walikiwa wamejiandikisha kupata huduma hiyo itakayohitimishwa Novemba, 29, 2024.