IDADI ya watu waliofariki dunia kutokana na ghorofa lililoporomoka, Kariakoo, jijini Dar es Salaam, imeongezeka na kufikia 29 baada ya miili tisa kubainika eneo hilo.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Thobias Makoba, akizungumza leo, amesema hayo mbele ya waandishi wa habari, jijini humo.
Pia, Makoba, ametangaza kurejea kwa biashara na kuanzia leo, Novemba 26, 2024 isipokuwa eneo la mtaa ambao ghorofa liliporomoka, Novemba 16, 2024.
Amesema miili mitatu kati ya hiyo, bado haijatambuliwa na kwamba majeruhi wawili wanaendelea kupatiwa matibabu.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED