Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mohamed Mchengerwa, (TAMISEMI), amesema kinachofanyika kuhusu ofisi za watendaji kudaiwa zimefungwa ni propaganda kwa kuwa zilikuwa wazi muda wote na wagombea walipaswa kurejesha fomu za maombi.
Aidha,amesema kanuni zina ruhusa ya kukataa rufaa lakini kinachoendelea sasa ni viongozi wa vyama kitaifa kulalamika huku wagombea wao wakiwa nyumbani hawakati rufaa kama kanuni zinavyoelekeza.
Akizungumza leo Novemba 12,2024,Waziri Mchengerwa amesema vyama hivyo vinafanya propaganda kwa kusambaza taarifa kwenye mitandao ya kijamii badala ya kufuata utaratibu wa kikanuni ambao umewekwa.
"Nilisikia eti Iringa,Kilimanjaro wagombea wa CHADEMA wameondolewa, hii si kweli,Novemba 14,2024 tutatoa taarifa za kina na ushahid wote.Vyama havikujiandaa na kupelekea kutoa nafasi kwa chama kimoja kugombea, Hai nafasi ni 60 na CCM Ilisimamisha wagombe wote ila CHADEMA ilisimamisha wagombea 30,sasa hawawezi kulingana na CCM,
"Hatua tuliyonayo ni ya propaganda ya siasa,waandishi mjitenge na propaganda hizi.Mfano diwani mstaafu aliandika kule Rufiji waliweka wagombea katika vijiji 32 na wote wakakatwa,jambo ambalo ni uongo,kwa kuwa Halmashauri ina vijiji 38,na CHADEMA kilisimamisha wagombea wawili,"amesema.
Mchengerwa amesema Dar es Salaam kuna mitaa 564 ila Diwani Mstaafu anasema kuna mitaa 600,lakini hawakusimamisha wagombea kwenye mitaa yote huku wakieneza taarifa za uongo.
Waziri huyo amesema kuhusu tafsiri ya umri kuna walioandika wamezaliwa mwaka 2024 maana yake haruhusiwi kugombea.
"Mfano Manispaa ya Kigoma Ujijii wagombea wa ACT Wazalendo walioenguliwa ni 11 na 58 walipitishwa,ila taarifa zao ni kwamba wagombea wote wameondolewa,11 walifuata taratibu za kanuni wakakata rufaa na watano walirejeshwa,na sita waliondolewa kwa changamoto ya umri,ukazi,kutojiandikisha, na udhamini,"amesema.
Aidha,Mchengerwa amabye ni Mbunge wa Jimbo la Rufiji amesema hata CCM kuna mgombea wao alijaza amezaliwa Oktoba 2024,na kwamba alienguliwa na kwamba hakuna upendeleo bali utekelezaji wa kanuni.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED