KATIBU wa NEC, Itikadi,Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla, amewataka wakulima na wafugaji wilayani Kiteto kutumia R4 za Rais Samia Suluhu Hassan kuishi kwa upendo na amani.
Aidha, amesema moja ya R4 za Rais Samia ni Mardhiano na alipokuwa wilayani Mvomero mkoani Morogoro mwezi uliopita kwenye ziara yake ya kikazi alizindua mardhiano ya wakulima na wafugaji.
Makalla aliyasema hayo leo Septemba 9 wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Engusero, Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara ikiwa ni sehemu ya ziara yake kukagua uhai wa chama,utekelezaji wa ulani,kusikiliza kero za wananchi na kuhamaisha ushiriki wa wananchi kwneye uchaguzi wa serikali za mitaa.
"Nawaomba mpendane na mheshimiane,mnategemeana sana mkulima yake ni mazao na mfugaji yake ni mifugo,kinachoendelea ni kutengeneza uhasama na kurudishana nyumba kiuchumi.Tutumie 4R za Samia kulindana na kuheshimiana,"amesema
Aidha, Makalla amesema mfugaji anategemea mazao ya mkulima,huku mkulima akitegemea mfugaji kupata kitowepo,hivyo watumie mardhiano kukaa pamoja kwa kuwa sote ni Watanzania.
MATUKIO YA UKATILI
Pia amelaani matukio la ulawiti baada ya tukio la mama na mwanaye kulawitiwa na kuuawa,na kuwataka viongozi wa dini kukemea.
Aidha,amewataka wananchi kutowaamini waganga kwa kuwa ni waongo na kusababisha matatizo kwenye jamii kwa kucheza na akili za watu.
"Imani za kishirikina zisitupelekee kutenda maovu,Jumuiya ya Wazazi,Jumuiya ya Wanawake kemeeni na kuendelea na kampeni ya kuouga vita matukio haya,"amesema.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED