EWURA yapewa tano utekelezaji mkakati wa nishati safi kwa vitendo

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 07:21 PM Nov 11 2024
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dk. James Mataragio.
Picha: Mpigapicha Wetu
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dk. James Mataragio.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imepongezwa kwa kutekeleza mkakati wa nishati safi ya kupikia kwa vitendo kwa kuweka mfumo wa huduma hiyo katika shule ya Sekondari Morogoro na Kituo cha Makazi ya Wazee cha Fungafunga mkoani Morogoro.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dk. James Mataragio ameyasema hayo leo kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Dotto Biteko kwenye kikao cha tatu cha Baraza la Pili la Wafanyakazi wa EWURA sambamba na uzinduzi wa mradi wa nishati safi na salama ya kupikia katika Shule ya sekondari Morogoro, uliotekelezwa na EWURA.
 
Naye, Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dk. James Andilile akitoa taarifa ya mradi huo, amesema ni utaratibu wa EWURA kurudisha kwa jamii kwa namna mbalimbali na kwamba, mradi huo utasaidia wanafunzi zaidi ya 700 wa Shule ya Sekondari Morogoro na Wazee zaidi ya 104 katika makazi yao Fungafunga.