Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule, amewataka viongozi waliopewa dhamana ya kuwaongoza wananchi hususani katika ngazi za mitaa,wakiwepo wenyeviti wa mtaa,makatibu na watendaji wa mitaa kuhakikisha wanatoa taarifa ya utekelezwaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuweka uwazi.
Mtambule aliyasema hayo jana Jijini Dar es Salaam kwenye kikao cha uwasilishwaji wa taarifa ya mafanikio ya Wilaya ya Kinondoni katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM,huku akiwapongezi viongozi ambao wanawajibika kikamilifu katika kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Kheri James,aliwataka viongozi kujenga mahusiano mazuri wao kwa wao pamoja na watu wanao waongoza ili kuweza kushirikiana katika ujenzi wa taifa kwa kufanya kazi kwa ustahimilivu
"Kuweni na mahusiano yaliyo bora na sambamba na mawasiliano mema kwa kila mtu haijarishi una cheo au mshahara ili kuboresha heshima ya Chama cha Mapinduzi ikiwa ni pamoja na kuweka heshima ndani ya nchi yetu." alisema James.
Kwa upande wa Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge, aliwaomba kufanyia kazi ilani ya Chama cha Mapinduzi pamoja ya kuonyesha ushirikiano kwa kila mtu ili kuleta haki na usawa katika jamii.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED