Benki Azania yazindua mfumo mpya wa kidijitali wa kibenki

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 08:52 AM Feb 14 2025
Mkuu wa Huduma za Benki Kidijitali wa Benki ya Azania, Vinesh Davda.
Picha: Mtandao
Mkuu wa Huduma za Benki Kidijitali wa Benki ya Azania, Vinesh Davda.

BENKI ya Azania imetangaza uzinduzi wa mfumo wake mpya wa kidijitali wa kibenki, AZANIA DIGITAL, ambao ni jukwaa la kisasa linalolenga kutoa suluhisho la kibenki linalofaa kwa wateja kote nchini.

Mfumo huo umeundwa kutoa huduma mbalimbali, ikiwamo benki kupitia simu, benki ya mtandaoni, huduma za wakala wa benki na huduma za benki kupitia WhatsApp, kuhakikisha wateja wanapata huduma rahisi na salama, popote walipo wakati wowote.

Katika hafla ya uzinduzi, Mkuu wa Huduma za Benki Kidijitali wa Benki ya Azania, Vinesh Davda, alisisitiza jinsi jukwaa hili litakavyobadilisha uzoefu wa wateja na kukuza ushirikishwaji kifedha nchini Tanzania. 

Alisema benki inakusudia kuboresha kiwango cha huduma za kifedha nchini kwa kutoa huduma zinazopatikana kirahisi na salama.

Davda alisisitiza kuwa jukwaa hili linakusudia kuleta mageuzi ya kifedha kwa wateja, hasa kwa kuzingatia mabadiliko ya kidijitali. 

Alisema, "Azania Digital Platform inahakikisha kwamba hakuna anayeachwa nyuma, kutoka kwa jumuiya za vijijini hadi wateja wa mijini, huduma za benki zinapatikana kwa urahisi na kwa haraka."

Davda alitoa wito kwa wateja kutumia mfumo huu mpya na kugundua manufaa yake, akisema kuwa uzinduzi wa Azania Digital ni hatua muhimu katika kuboresha huduma za kifedha na ushirikishwaji kifedha kwa Watanzania wote.