Kapinga ashiriki kikao cha mawaziri wa kisekta Arusha

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 05:48 PM Feb 14 2025
Kapinga ashiriki kikao 
cha mawaziri wa kisekta 
Arusha.
Picha: Mpigapicha Wetu
Kapinga ashiriki kikao cha mawaziri wa kisekta Arusha.

Naibu Waziri Nishati, Judith Kapinga leo Februari 14, 2025 amemuwakilisha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati,Dk. Doto Biteko kwenye Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la kisekta la Nishati, Petroli na Madini la Jumuia ya Afrika Mashariki Jijini Arusha.

Baraza la kisekta limekutana kujadili miradi ambayo inatekelezwa ambayo ni pamoja na mradi wa kufua umeme wa Nsongezi utakaotekelezwa na Nchi za Tanzania, Rwanda na Uganda ambapo Mawaziri husika watasaini Hati ya Makubaliano (MoU) ya utekelezaji wa Mradi huu. 

Aidha, Baraza hili linasimamia Kongamano na Maonesho ya 11 ya Petroli ya Jumuiya ya Afrika  Mashariki ambalo litafanyika tarehe 5 hadi 7 Machi 2025 Jijini, Dar es Salaam. 

Uenyeji wa Tanzania katika kongamano hilo unatokana na maamuzi ya mkutano wa 16 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta lililofanyika Mwezi Februari 2024  ambalo liliamua Tanzania kuwa Mwenyeji wa Kongamano hilo.