Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, amelazwa hospitalini leo Ijumaa asubuhi kwa ajili ya vipimo na kuendelea na matibabu ya ugonjwa wa mkamba (bronchitis) unaomsumbua, Vatican imethibitisha.
Kwa mujibu wa taarifa ya Vatican, baada ya kumaliza ibada yake ya kawaida kwa hadhira yake, Papa Francis alipelekwa katika Hospitali ya Policlinico Agostino Gemelli kwa ajili ya uchunguzi wa afya na matibabu zaidi katika mazingira ya hospitali.
Papa Francis, mwenye umri wa miaka 88, amekuwa akiongoza Kanisa Katoliki tangu mwaka 2013 na katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, amekumbwa na changamoto mbalimbali za kiafya, ikiwemo mafua na matatizo mengine ya mfumo wa kupumua.
Licha ya matatizo ya kiafya, Papa ameendelea na ratiba zake za kila siku katika makazi yake ndani ya Vatican. Kabla ya kwenda hospitalini leo, alikutana rasmi na Waziri Mkuu wa Slovakia, Robert Fico.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED