Kituo cha Ubia chaendesha mafunzo na uibuaji miradi Songwe

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 01:56 PM Feb 15 2025
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja.
Picha: Mtandao
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja.

Kituo cha Ubia kiliendesha zoezi la mafunzo na uibuaji miradi kwa watendaji hitajika wa Halmshauri ya Wilaya ya Songwe mkoani Songwe.

Kwenye mafunzo hayo, wataalam kutoka Kituo Cha Ubia waliendesha mafunzo kuhusu kazi za kituo, dhana ya Ubia kwa ujumla wake, pamoja na kuratibu zoezi za kuibua miradi yenye sifa za ubia.

Aidha, watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe walifurahi kupata mafunzo hayo na kutoa ushirikiano mkubwa kwenye zoezi la kuibua miradi pendekezwa. 

Uongozi wa Halmshauri umehakikishia kituo cha Ubia kuwa, uko tayari muda wote kwa ajili ya hatua zitakazofuata.