Mama Mzazi wa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) bara, John Heche amesema hakupenda mwanawe kuingia katika siasa kwa kuhofia misuko suko itakayompata.
Akizungumza na chombo kimojawapo cha habari nchini, amesema wakati mwanawe huyo akigombea udiwani kwa mara ya kwanza hakuwa karibu na hivyo kushindwa kumzuia kugombea.
“Alipopata udiwani kwa mara ya kwanza nilimshukuru Mungu kwamba aliupata mimi nikiwa sipo, ningekuwepo ningemzuia kwa sababu kazi ya siasa mimi sikuipenda niliona ina misukosuko mingi” amesema Mama huyo.
“Wakati akiwa diwani kwa mara ya kwanza tulitupiwa vitu nje, kwa hiyo sikuipenda lakini kwa sasa namshukuru Mungu kwa ajili ya usimamizi wake kwa familia”.
“Hata alipogombea ubunge nilijaribu kumzuia asigombee ubunge maana yake tena ilileta misukosuko mingi sana ,lakini hakukubali na mimi nikakubaliana naye, kitu pekee nilichoweza kufanya ni kumuombea” amesema
"Kuna siku tulirushiwa sijui alikuwa mbwa yule akiwa amekufa, akarushwa kwenye geti tukamkuta ndani, kwahiyo nikawa naogopa sana vitu hivyo" ameongeza.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED