Kampeni michuano Euro yaanza kutoa washindi

By Faustine Feliciane , Nipashe Jumapili
Published at 08:42 AM Jun 02 2024
Meneja wa Wateja wa Maalum wa Tigo Pesa, Mary Ruta.
Picha: Mtandaoni
Meneja wa Wateja wa Maalum wa Tigo Pesa, Mary Ruta.

SIKU chache baada ya kuzinduliwa kwa Kampeni ya Michuano ya Ulaya 'Zigo la Euro 2024', tayari washindi wameanza kupatikana.

Michuano ya Euro 2024 inatarajiwa kuanza hivi karibuni nchini Ujerumani, na baadhi ya mashabiki watapata fursa ya kwenda kushuhudia michuano hiyo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa Wateja wa Maalum wa Tigo Pesa, Mary Ruta, alisema katika kampeni hiyo watatoa zawadi mbalimbali ikiwamo safari ya kwenda kushuhudia michuano hiyo.

Ruta alisema washindi hao wanaingia katika droo kwa kufanya miamala au kubashiriki mechi kupitia Parimatch.

 "Leo (jana) tumepata washindi wa kwanza ambao wamejishindia zawadi mbalimbali.

Alisema washindi hao wamepata zawadi ya jokofu, televisheni, fedha na tiketi moja ya kwenda kushuhudia michuano hiyo.

Aliwataja washindi hao ni pamoja na Maurin Shirima ambaye alijishindia televisheni, Ramadhan Mrutu, amepata  tiketi ya kwenda Ujerumani huku zawadi ya Sh. milioni moja ikienda kwa Fredy Mlay.