Uwekezaji watoa fursa mpya ya ajira kwa vijana

By Maulid Mmbaga , Nipashe Jumapili
Published at 02:26 PM Sep 01 2024
Muanzilishi wa kamapuni ya YLM, raia na muwekezaji kutoka nchini China Mishel, kulia akielezea fursa za ajiri kwa vijana vinazopatikana katika kampuni yake.
Picha Maulid Mmbaga.
Muanzilishi wa kamapuni ya YLM, raia na muwekezaji kutoka nchini China Mishel, kulia akielezea fursa za ajiri kwa vijana vinazopatikana katika kampuni yake.

ZIARA ya Rais Samia Suluhu Hassan nchini China imeendelea kuzaa matunda baada ya wawekezaji kutoka taifa hilo kuendelea kumiminika nchini kwaajili ya kuwekeza kwa kuanzisha viwanda ambavyo vinatengeneza ajira kwa vijana.

Siku chache zilizopita Rais Samia alifanya ziara ya kikazi nchini China kwa lengo la kwenda kuvutia wawekezaji kwa kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji zinazopatikana nchini, ambako alitoa wito kwa wadau kuja kuzichangamkia.

Akizungumza leo mkoani Dar es Salaam, raia na muwekezaji kutoka China aliyejitambulisha kwa jina la Mishel, amaye ni muanzilishi wa kampuni ya YLM, amesema ameamua kuja Tanzania kuwekeza baada ya kuona kuna fura kubwa katika upande wa chakula.

"Miaka michache iliyopita niliwahi kuishi Tanzania, nilibaini kuwa kuna kitu watu wanakosa hasa kwa upande wa 'snaks' na nimeamua kuja kufungua kiwanda cha karanga, na hii itakuwa fursa kwa watu wengi kupata kazi, na hadi kufikia sasa nimeajiri wafanyakazi zaidi ya 20," amesema Mishel.

Ameongeza kuwa kupitia kiwanda hicho siku za baadae atapanua wigo na kuzalisha bidhaa zingine mbalimbali kulingana na uhitaji utakaokuweko kwa wakatu huo, huku akisisitiza watanzania kuchangamkia fursa hiyo kwaajili ya kuendesha biashara ya uwakala na kuongeza kipato chao.

Shamsa Fodi ambae ni balozi wa kampuni hiyo, amesema uwekezaji huo ni fursa kwa Tanzania kwakuwa itapunguza idadi ya vijana wanaokaa vijiweni kwakutokuwa na ajira, kwasababu watapata kazi zitakazowasaidia kuingiza kipato.

Amesema uwekezaji huo pia unalenga zaidi vijana na kwamba umeshatengeneza ajira kwa wengi ambao kwa sasa wanaendesha maisha yao kupitia hapo. Akieleza kuwa YLM iko kwaajili ya kumpa fursa kijana wa Kitanzania.

"Muache kukaa vijiweni mje mfanye kazi, kampuni ni kubwa na bado inahitaji vijana wengi zaidi kuja kufanya kazi, utaenda kuuza bidhaa ambayo hutapata shida kuielezea, na tunatoa wito kwa wafanyabisahara wa ndani kutumia fursa hii kwaajili ya kujipanua kibiashara," amesema Shamsa.