Polisi Kenya kuchunguza maiti zilizofungwa kwenye viroba

By Mwandishi Wetu , Nipashe Jumapili
Published at 03:16 PM Jul 14 2024
Utepe wa kuonesha hali ya hatari (uchunguzi) katika eneo husika, kwa ajali ya polisi kufanya majukumu yao.
Picha: Mtandao
Utepe wa kuonesha hali ya hatari (uchunguzi) katika eneo husika, kwa ajali ya polisi kufanya majukumu yao.

JESHI la polisi nchini Kenya, limesema linachunguza tukio la maiti zilizokatwakatwa na kufungwa kwenye viroba na kisha kutupwa kwenye dampo la takataka jijini Nairobi.

Taarifa kutoka Idara ya polisi nchini humo, zilieleza uchunguzi unalenga kubaini kama askari wake wanahusika na tukio hilo au watu wengine,

Jumla ya maiti 10 zilipatikana juzi zikiwa zimetupwa katika dampo hilo lililoko eneo la Mukuru, ambalo linakaliwa na watu maskini katika jiji hilo.

Idadi hiyo inaweza kuongezeka  kutokana na juhudi ya kutafuta miili mingine zilikatizwa baada ya watu wengi kukusanyika eneo hilo na ilibidi kutawanywa na mabomu ya machozi.

Wiki mbili zilizopita vijana wanaojiita Gen Z, waliitisha maandamano kupinga muswada wa fedha ambayo yalivunjwa na polisi ambao walitumia nguvu ya ziada.

Kutokana na maandamano hayo, Mkuu wa polisi nchini humo, Inspekta Jenerali Japhet Koome alitangaza kujiuzulu.

Tukio hilo la kupatikana kwa miili hiyo katika mifuko ya plastiki, linarudisha kumbukumbu mbaya katika Mto Yala baada ya maiti 40 kupatikana zikiwa katika hali hiyo.

Mashirika ya haki za binadamu yameshuku kuwa miili hiyo ni ya wahanga waliouawa wakiwa mikononi mwa vyombo vya dola.

Mamlaka Huru ya Kusimamia Polisi (IGen Z,) pia inachunguza madai ya utekaji nyara na kukamatwa kinyume cha sheria kwa waandamanaji ambao walitoweka kufuatia maandamano yaliyoenea dhidi ya serikali.

RFI