Kampuni bora 130 Afrika zatuzwa

By Christina Mwakangale , Nipashe Jumapili
Published at 08:50 AM Jun 02 2024
Miongoni mwa washindi, mshindi wa jumla akiwa ni Petrol Group Tanzania, na Mansoor industries Limited na  Sunking -Green Platent.
PICHA: MPIGAPICHA WETU
Miongoni mwa washindi, mshindi wa jumla akiwa ni Petrol Group Tanzania, na Mansoor industries Limited na Sunking -Green Platent.

KAMPUNI 130 zimetunukiwa tuzo, baada kuhimili ushindani katika soko la dunia, ili kuzipa chachu, kuyaongezea ufanisi wa uzalishaji wa bidhaa bora na zenye viwango na tija katika maendeleo na ukuaji wa uchumi ndani barani Afrika.

Tuzo hizo zijulikanazo Tuzo za Kampuni. Ora Barani Afrika m (ACOYA), zimeandaliwa na The Global CEOs Institute kwa kushirikiana na Eastern Star Consulting Group Tanzania.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Eastern Star Group of Tanzania, Deogratius Kilawe, amesema hayo leo, kwenye hafla ya kutunuku tuzo hizo, kwa mwaka 2024 iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

"Lengo ni kutambua mchango mkubwa wa kampuni zinazofanya vizuri barani Afrika na kuwapongeza na kuwapa moyo, ili waendelee kufanya vizuri zaidi, kuhudumia soko la Afrika.

“Kwa kutoa huduma na bidhaa zenye ubora wa hali ya juu zinazoweza kupambana na soko la dunia, pamoja na kukuza uchumi wa nchi za Afrika kwa ujumla,” amesema.

Kilawe amesema kuwa pamoja na mambo mengine, huu ni msimu wa pili wa tuzo kama hizo, ambazo zilianza mwaka jana na kuleta mafanikio na kuzileta pamoja kampuni kubwa Afrika, kujadili mambo mbalimbali yatakayosaidia kukuza uchumi.

Pia aliongeza kuwa, mwaka huu ni zaidi ya nchi 20 na kampuni 700 yameshiriki katika tuzo  hizo, huku 130 zikiibuka bora na kutuzwa, ili kuchochea ufanisi na katika uzalishaji wa bidhaa na huduma.

Miongoni ma viongozi waliohudhuria tuzo hizo, ni Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Shabani Omary pamoja na viongozi mbalimbali.