HABARI mbaya mwaka mpya wa 2025, ni hizi unadaiwa umekaribishwa na maradhi yanayotokana na virusi vikali kuliko UVIKO 19.
Ni mlipuko mpya wa virusi nchini China vikipewa jina la ‘human metapneumovirus’ (HMPV) na sasa kikubwa ni kujua dalili, vidokezo vya kuzuia na namna ya kujitibu.
Watoto wadogo, watu wazima, wazee na wale walio na kinga dhaifu kutokana na magonjwa yasiyoambukiza, wako katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa huo wa HMPV.
Kwa mujibu wa Mtandao wa NDTV wa India, ripoti na taarifa za kuwapo maradhi hayo zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii, zikisema hospitali zimejaa watu walioambukizwa na maeneo ya kuchomea maiti yamezidiwa kutokana na vifo vingi.
Taarifa zinasema India pia inafanya uchunguzi wa kuwapo kwa maradhi hayo na imeshauri raia kuchukua tahadhari. Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wanadai kwamba virusi vingi, ikiwa ni pamoja na mafua HMPV, mycoplasma pneumoniae na COVID-19, vinazunguka nchini China.
Anaongeza kuwa: “Magonjwa yanaonekana kuwa mabaya zaidi na yanaenea kwa kiwango kidogo ikilinganishwa na mwaka uliopita," anasema, licha ya kwamba kuna madai kwamba China imetangaza hali ya hatari hasa eneo la kaskazini ambako maradhi hayo yanatikisa.
Taarifa zinasema India pia inafanya uchunguzi wa kuwapo kwa maradhi hayo na imeshauri raia kuchukua tahadhari. Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wanadai kwamba virusi vingi, ikiwa ni pamoja na mafua HMPV, mycoplasma pneumoniae na COVID-19, vinazunguka nchini China.
HMPV husababisha dalili zinazofanana na mafua. Kwa kawaida virusi huathiri mfumo wa juu wa upumuaji ambao ni pua, mdomo, koromeo na koo na ‘larynx’ au kisanduku cha sauti, hivyo sauti hukwama.
Lakini wakati mwingine huweza kusababisha maambukizo ya njia ya chini ya upumuaji kwenye sehemu ya mfumo wa kupumua ambayo ni pamoja ‘koromeo au trakea, pia ni njia kubwa za kupeleka hewa kwenye mapafu na zile ndogo . Mishipa ya hewa ndani ya mapafu (bronchioles) na ‘alveoli’ ambayo ni mifuko ya hewa ndani ya mapafu inayobadilisha hewa chafu au gesi ya kaboni na kuchukua oksjeni wakati wa kupumua.
HMPV inadaiwa ni maradhi ya kawaida zaidi katika majira ya baridi na kwenye hatua za mwanzo za msimu wa machipukizi (spring).
TAHADHARI
Dalili za metapneumovirus ni sawa na za mafua au homa ya kawaida. Inaweza kuenezwa kutoka kwa mtu aliyeambukizwa hadi kwa wengine kupitia kukohoa, kupiga chafya au kugusana au kushika majimaji za mwili kama makamasi, mate na damu za mtu mgonjwa.
Baadhi ya dalili za kawaida ni pamoja na kikohozi homa kali, kuziba au kubanwa pua, maumivu makali kooni, kushindwa kupumua na kukosa hewa.Ugonjwa hulipuka baada ya siku tatu hadi sita baada ya maambukizi kutegemea ukali wa virusi na uimara wa kinga ya mwili.
JITAMBUE
Ni nani aliye katika hatari kubwa zaidi? Jibu ni watoto wadogo, watu wazima, wazee na wale walio na udhaifu unaodhoofisha kinga.
Wako katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa huo wa HMPV. Wakati mwingine HMPV inaweza kusababisha ugonjwa mbaya ambao unalazimisha kulazwa hospitalini. Unaambatana na ‘bronkaitisi’, nimonia, pumu na hata maambukizi masikioni.
KUJIKINGA
Vidokezo vya kuzuia maambukizi ni pamoja na kunawa mikono kwa sabuni na maji kwa angalau sekunde 20 ili kudhibiti kuenea.Kufunika mdomo na pua wakati wa kukohoa au kupiga chafya, kutumia au kuvaa barakoa na kuepuka kushirikiana au kuchanganyika na wale ambao ni wagonjwa .
Kuacha kugusa macho, pua na mdomo kwa mikono ambayo haijaoshwa na kufanya mazoezi lakini pia kujitenga au kujiweka karantini ikiwa ni mgonjwa. Hivi sasa, hakuna tiba maalum wala dawa ya kuzuia virusi au chanjo ya kukinga na HMPV.
Mtandao wa Cleveland Clinic, unaeleza kuwa Human metapneumovirus (HMPV) ni virusi ambavyo kwa kawaida husababisha dalili zinazofanana na homa na mafua.
Iwapo umeathirika unaweza kukohoa au kupumua kwa shida , kuwashwa pua na kuumwa na koo kukereketa pia. Aidha, si wakati wote wote ugonjwa au mafua yanakuwa makali.
Hata hivyo, watoto wadogo, watu wazima zaidi ya miaka 65 na watu walio na maradhi yanayonyong’onyeza kinga wako kwenye hatari kubwa ya ugonjwa huo mbaya.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED