WAASI M23; Marekani yafikiria vikwazo dhidi ya Rwanda, DRC

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 07:19 PM Feb 07 2025
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Félix Tshisekedi na mwenzake wa Marekani, Donalgd Trump
Picha: Mtandao
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Félix Tshisekedi na mwenzake wa Marekani, Donalgd Trump

MAREKANI imezionya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kwamba upo uwezekano wa kuwawekea vikwazo maofisa wao.

Kabla ya mkutano wa kilele uliokusudiwa kushughulikia mzozo wa Mashariki mwa Congo, kw mujibu wa barua ya kidiplomasia iliyoonekana na Reuters, leo, Ijumaa.

DRC na Rwanda, wamekuwa wakilaumiana kwa mzozo ulioanza tena Mashariki mwa Congo, huku waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda, wakiuteka mji mkuu wa mkoa Goma na kuendelea katika maeneo mengine zaidi.

Rais wa Rwanda, Paul Kagame na mwenzake wa Marekani, Donald Trump
Ujumbe wa kidiplomasia uliotumwa Ijumaa na Marekani kwenda Kenya, ambayo ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na imekuwa mpatanishi katika mzozo huo, ulisema utulivu katika eneo hilo utahitaji jeshi la Rwanda kuondoa vikosi vyake na silaha nchini DRC.

"Tunapoweka matakwa haya kwa pande zote mbili, tutazingatia kuweka vikwazo dhidi ya wasio washirika, pamoja na maofisa wa jeshi na serikali katika serikali zote mbili," taarifa hiyo ilisema.

BBC