CCM Songea kuandamana kuunga mkono Mkutano Mkuu, Samia tena

By Gideon Mwakanosya , Nipashe
Published at 09:36 AM Feb 07 2025
Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu, Emmanuel Nchimbi
Picha Mtandao
Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu, Emmanuel Nchimbi

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Songea Mjini na Vijijini mkoani Ruvuma, kinatarajia kufanya maandamano yakifuatiwa na mkutano, lengo likiwa ni kuunga mkono maazimio ya Mkutano Mkuu CCM, uliofanyika Dodoma.

Mkutano huo, ulimthibitisha Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kuwa mgombea pekee wa urais kwenye Uchaguzi Mkuu, unaotarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu.


Kadhalika, mkutano huo, ulimpitisha Dk. Emmanuel Nchimbi, kuwa mgombea mwenza ambaye wa rais. nchini kwa sasa ni Katibu Mkuu wa CCM Taifa.


Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Katibu wa CCM wa Wilaya ya Songea Mjini, James Mgego, alisema kuwa CCM Wilaya hiyo, kinaunga mkono mkutano huo utakaofanyika Februari 8, mwaka huu.


Alisema mkutano huo unatarajiwa kufanyiaka viwanja vya Matarawe, Manispaa ya Songea na kuhudhuriwa na wananchi pamoja na wanachama wengine wa CCM.

CCM Songea kuandamana kuunga mkono Mkutano Mkuu, Samia tena
Alisema kuwa mgeni rasmi wa mkutano huo, anatarajiwa kuwa ni mmoja wa viongozi wa ngazi za juu wa CCM. Hata hivyo hakubainisha jina.


“Nawaomba wananchi kuona umuhimu wa kuhudhuria mkutano huu, kama ilivyo ada kwa ujio wa viongozi wa ngazi ya kitaifa na kufurika uwanjani.


“Maandamano yataanza majira ya asubuhi yakianzia London, Kata ya Lizaboni, Msamala pamoja na kwenye ofisi za chama Mkoa na yataongozwa na jumuiya zote za chama vijana, Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), pamoja na Jumuiya ya Wazazi.