Wanawake waja na ‘Hongera Samia Event’

By Christina Mwakangale , Nipashe
Published at 06:59 PM Feb 07 2025
Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Foundation, Jackline Marwa, akizungumza na waaandishi wa habari
Picha: Christina Mwakangale
Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Foundation, Jackline Marwa, akizungumza na waaandishi wa habari

TAASISI ya Jamii Foundation kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, pamoja na wanawsake wa mkoa huo, wameandaana kongamano pamoja na matembezi kuunga mkono mafanikio ya Rais Samia Suluhu Hassan, hasa katika sera yake ya nishati safi ya kupikia.

Mkurugenzi wa Mtendaji wa taasisi hiyo, Jackline Marwa, ameyasema hayo leo, Februari 7, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kwamba kongamano hilo litajulikana kama Hongera Samia Event.

Amesema kongamano hilo litakalowakutanisha washiriki takribani 1,000 mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, litafanyika Februari 27, mwaka huu.

Wanawake waja na ‘Hongera Samia Event’
Mkurugenzi Mtendadi wa Caliber First Group, Sylvia Mkomwa, amesema wanaiunga mkono taasisi hiyo ili kutambua mchango wa Rais Samia, akiwa mwanamke anayebeba maono ya wanawake wengine, kwwneye sekta ya nishati, afya na elimu.

“Tunafuraha kuwa na Jamii Foundation kupongeza kazi ya Rais na tunaona matokeo mbalimbali. Tunashirikiana na ili kufanya shughuli za kimaendeleo. Kwa jukwaa hili tunaoneaha mfano kupitia Rais kwamba wanawake wana wajibu mkubwa.”