Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu William Lukuvi amemshukuru na kumpongeza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa kuendelea kusimamia na kuratibu shughuli za Serikali kwa weledi mkubwa.
Waziri Lukuvi ametoa pongezi hizo wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu uliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi hiyo Ngome Jijini Dododma leo Februari,07, 2025.
Amesema kuwa kazi ya Waziri Mkuu kwa Mujibu wa Katiba ni kuratibu shughuli zote za Serikali na chini yake yupo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati na watendaji wa Ofisi yake ambao wanatekeleza majukumu hayo kwa weledi na ufanisi mkubwa.
“Wakati wa uratibu wa shughuli za Maafa watendaji mmefanya kazi kwa ushirikiano Mkubwa chini ya Uongozi wa Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na mambo yameenda vizuri nchi nzima,” amesema Waziri Lukuvi
Aidha amefafanua kuwa kazi ya Ofisi ya Waziri Mkuu ni kuratibu Serikali ili kuwafahamisha namna Serikali inavyoendelea kutekeleza majukumu na kuhudumia wananchi.
"...Kwa kuwa tuna nafasi ya kupata taarifa na kuzifanyia uchambuzi ili kujulisha umma kwa njia mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari basi tuendelee kuratibu vyema taarifa na kuzitoa kwa usahihi ndiyo jukumu letu kubwa na la msingi lazima tujipange ili ziweze kutoka kwa wakati amesema,” Waziri Lukuvi.
Naye Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Dk. Jim Yonazi katika maneno ya utangulizi amesema Viongozi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wamewatengeneza mazingira mazuri kwa watendaji kufanya kazi kwa furaha na amani.
Pia ameahidi kuimarisha ushirikiano miongoni mwao ili kuyafikia maelengo ya ofisi na Serikali kwa ujumla.
"Tuimarishe ushirikiano miongoni mwetu ili kazi zetu ziende kwa wepesi na ufanisi kwa kuamini kila mmoja ana mchango chanya kuhakikisha malengo yanatimia," amesema Dk. Yonazi
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED