Balozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,Said Mshana, amempokea Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat, aliyewasili nchini Tanzania alfajiri ya Februari 8, 2025.
Ziara yake inalenga kuiwakilisha Umoja wa Afrika katika Mkutano wa Dharura wa Pamoja wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika baadaye.
Mkutano huo unalenga kujadili na kutafuta suluhisho kuhusu hali ya ulinzi na usalama katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED