Maabara ya Mkemia yatoa elimu upimaji vinasaba, jinsi tata 77

By Mary Geofrey , Nipashe
Published at 10:48 AM Jul 05 2024
Maabara ya Mkemia yatoa elimu upimaji vinasaba, jinsi tata  77
Picha: Mpigapicha Wetu
Maabara ya Mkemia yatoa elimu upimaji vinasaba, jinsi tata 77

MAMLAKA ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) imewataka wananchi kujitokeza kupata elimu sahihi ya shughuli wanazofanya.

Mwakilishi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa serikali (GCLA) Stafford Maugo, ametoa rai hiyo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda lao katika Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba).

Amesema kupitia maonyesho hayo watawaelezea aina ya chunguzi wanazofanya kwa kushirikiana na taasisi binafsi na serikali.

"Mfano Polisi akikamata dawa za kulevya, bangi na mirungi atazileta hapa kwenye maabara ya rufaa kwaajili ya kufanya uhakiki kama ni kweli ni dawa za kulevya au kitu kingine," amesema.

Maugo ambaye pia ni mkaguzi wa kemikali amesema pia kesi za ubakaji askari wanapokamata vielelezo na kuvipeleka kwenye maabara lengi ni kumfahamu muhusika wa tukio hilo ili kuchukua hatua stahiki.

Amesema pia kuna huduma za vinasaba wanapima ili kutatua migogoro ya familia kuhusu uhalali wa watoto.
Maugo amesema pia wanachunguza kuhusu jinsi tata kwa watoto waliozaliwa na jinsia mbili lengo ni kusaidia madaktari kutambua jinsi iliyotawala.

"Vipimo hivyo vitamsaidia daktari kuondoa ile jinsi ambayo haijatawala," amesema Maugo.

Amesema katika maonesho hayo wanawasaida wateja wa kemikali kujisajili na kuingia kwenye mfumo wa maalum wa huduma za kemikali.