Serikali inachunguza ajali ya moto Siha

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 12:36 PM Jul 08 2024
 Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel
PICHA: MPIGAPICHA WETU
Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel

Serikali inaendelea kuchunguza chanzo cha moto kilichotolea kata ya Ngarenairobi Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro na kuhakikisha wananchi wanapata huduma muhimu.

Hayo yamesemwa leo na Mbunge wa Jimbo la Siha (CCM) ambaye ni  Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel, wakati wa mkutano wake na wananchi wa kijiji  cha Roseline kata ya Ndumeti wilayani Siha.

Dk. Mollel alipofika kata ya Ngarenairobi  aliwafariji wahanga hao huku akiwahakikishia watoto  wao kuendelea na masomo na huduma muhimu kwa wananchi watapatiwa.

Amesema wananchi ambao wamepata ajili ya kuunguliwa nyumba zao wametakiwa kuwa watulivu kwa kuwa serikali inaendelea kuchunguza tukio hilo ili waendelee na maisha yao ya utafutaji.

Tukio hilo lilitokea Julai 6 mwaka huu nyumba yenye vyumba 11 vya wapangaji viliteketea kwa moto na kusababisha hasara.