Tani 1,000 za ufuta zauzwa Kibiti, ni mnada wa nne wakulima kicheko

By Yasmine Protace , Nipashe
Published at 05:10 PM Jul 08 2024
Tani 1,000 za ufuta zauzwa Kibiti, ni mnada wa nne wakulima kicheko
Picha: Mpigapicha Wetu
Tani 1,000 za ufuta zauzwa Kibiti, ni mnada wa nne wakulima kicheko

ZAIDI ya tani 1,000 za ufuta zimeuzwa katika mnada wa nne,uliofanyika Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani. Hayo yalisemwa na Meneja wa CORRECU Mkoa wa Pwani,Hamis Mantawela,wakati akizungumza na waandishi wa habari.

" Huu ni mnada wa nne,ambapo tumeuza tani 1,100 kwa bei ya wastani ya kilo moja kwa shilingi 3280.13," alisema.

Aliongeza kuwa,bei ya juu ilikuwa kwa kilo moja shilingi 3330,bei ya chini  ilikuwa shilingi 3243 huku bei ya wastani ilikuwa shilingi 3280.13.

Aliongeza kuwa mnada huo,uliofanyika ulikuwa ni mnada wa nne,ambapo ufuta wote ziliuzwa tofauti na minada mitatu iliyofanyika korosho zilibaki.

Hata hivyo,ameishukuru serikali kwa kusikiliza kilio cha wakulima wa ufuta na kufanikiwa kwa kuboreshwa kwa mfumo huo.

" Wakulima waliulalamikia mfumo wa TMX ambao ulikuwa humuoni mnunuaji hivyo mnada kufanyika na kusababisha baadhi ya wanunuzi kuchukuwa bidhaa kidogo na kuziacha nyingine," alisema.

Aliongeza kuwa baada ya kupelekwa malalamiko ya wakulima kwa Waziri wa Kilimo Hussein Bashe,suala hilo mfumo TMX limeboreshwa ambapo bidhaa itauzwa godauni kwa godauni na kila mnunuzi atakayechukuwa bidhaa atalazimika kuchukuwa mizigo yote.

" Leo ufuta umeuzwa wote uliokusanywa,tofauti na miradi ya nyuma mitatu ambayo ilifanyika,ufuta uliuzwa kidogo huku mwingine ukibaki," alisema.

Tifu Nguluki mkulima wa ufuta alisema kuwa,bei haijafikia nzuri Kama wakulima walivyotaka.
Alisema mfumo wa TMX  haujuwa mzuri kutokana na mzigo kubaki.

Alisema huu mfumo ulioboreshwa umesaidia ufuta wote kuisha.

Aliongeza kuwa,kwanza anawashukuru viongozi wao wa CORRECU ambao walipeleka malalamiko yao Fodoma ambapo majibu mazuri yamerudishwa.

Pia alisema wanamshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa ambapo zamani ufuta uliuzwa kilo shilingi 800 sasa umepanda bei.

Alisema serikali sasa imesimama katika nafasi yake kwa kutatua tatizo la wakulima.

Aliongeza kuwa hata kwa upande wa wakulima kwa sasa pembejeo zimeanza kutolewa.