Makonda ataka ushirikiano na Asasi za Kiraia

By Beatrice Shayo , Nipashe
Published at 01:16 PM Jul 08 2024
news
PICHA: MPIGAPICHA WETU
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, ameyakaribisha mashirika na asasi za kiraia zilipo mkoani Arusha, kushirikiana kwa lengo kuongeza kasi zaidi ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Makonda ametoa kauli  leo wakati wa mkutano wake na wadau wa mashirika na asasi hizo zinazoshughulika na maendeleo ya huduma za jamii.

"Niwakaribishe kuitumia ofisi ya Mkoa kama sehemu ya ofisi yenu jambo lolote unaloweza kuwa nalo, Mtu yeyote mwenye shughuli ndani ya mkoa wa Arusha, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Ofisi ya mkuu wa wilaya ni ofisi yako.Unapaswa kwenda kifua mbele na kuomba mahitaji yako ili ufanikishe kile unachokifanya ambacho sisi tunaamini ndicho kinachoweza kuleta tija kwenye maisha ya wananchi tunaowaongoza." ameongeza Makonda.

Katika Mkutano huo wadau wa asasi 1,224 wanatoa maoni na changamoto zao kwa Makonda ambaye ameahidi kuzifanyia kazi katika kuongeza ufanisi na kasi ya utendaji wao wa kazi na kuweka mazingira rafiki ya mashirika hayo katika kuwatumikia wananchi jijini Arusha.