MENEJA Programu wa Shirika la Maendeleo ya Jamii la Tusonge CDO, Lawi Msemwa, ameshinda tuzo ya utendaji bora kwa mwaka 2024 (Best Performance), huku Ofisa Takwimu, Chris Monyo, akitwaa tuzo ya utendaji mzuri inayotolewa na Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika hilo, linalofanya kazi zaidi na makundi ya jamii ya pembezoni.
Wengine waliotwaa tuzo ya ‘punctuality’ kazini, ni Kaimu Ofisa Rasilimali Watu wa Shirika hilo, Lilian Maro, Dereva ambaye ni kiraka katika menejimenti na miradi, Ainea Petro na mhudumu Hossiana Minja.
Akizungumza jana wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi hizo kwa niaba ya Bodi ya Shirika la Tusonge CDO, lililoko Moshi, mkoani Kilimanjaro, Mkurugenzi Mtendaji, Aginatha Rutazaa, amesema menejimenti imeanzisha tuzo hiyo ili kuchochea uwajibikaji na ufanisi kazini.
Zaidi Mkurugenzi huyo wa Tusonge CDO, Aginatha Rutazaa anasema, pia menejimenti ya Shirika hilo imwatoa tuzo nyingine za jumla kwa utendaji kazini kwa wafanyakazi 15 ili kuwatia moyo na kuchochea uwajibikaji mwaka ujao….
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED