Kiongozi wa ACT Wazalendo ampongeza Lissu kwa ushindi

By Sabato Kasika , Nipashe
Published at 05:10 PM Jan 22 2025
KIONGOZI wa Chama cha ACT wazalendo, Dorothy Semu.
Picha: Mtandao
KIONGOZI wa Chama cha ACT wazalendo, Dorothy Semu.

KIONGOZI wa Chama cha ACT wazalendo, Dorothy Semu amempongeza mwenyekiti mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tundu Lissu na kumtakia kazi njema.

Mbali na kumpongeza Lissu, Kiongozi huyo poa amempongeza kwa kukamilisha uongozi na kuachia demokrasia ichukue mkondo wake ndani ya chama hicho na kumtakia heri ya maisha ya ustaafu.

Dorothy ametoa pongezi` hizo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii baada ya Lissu kushinda nafasi hiyo katika uchaguzi uliofanyika usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam.

"Nakupongeza Tundu Lissu kwa Kushinda uchaguzi na kuwa mwenyekiti wa chama chako cha CHADEMA. Kuchaguliwa kwako kunakufanya pia uwe Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD)," ameandika Dorothy.

Dorothy ameendelea kuandika; "Nikiwa makamu wako huko, nakukaribisha sana katika uongozi wa TCD. Nikiwa Kiongozi wa ACT Wazalendo nakuhakikishia ushirikiano wa dhati katika kupigania demokrasia ya nchi yetu."