MSANII wa Mziki wa Kizazi Kipya, Deo meta maarufu De Master amewaomba mashabiki zake wamuunge mkono kupitia wimbo wake mpya aliouachia hivi karibuni.
De master ameliambia gazeti hili jana kwamba mbali na wimbo huo, kwa sasa anaandaa mwingine anaotarajia kuuachia siku chache zijazo.
“Mashabiki zangu nipo kitambo kwenye gemu, ninafata nyayo za mama angu ambae pia alikuwa msanii wa nyimbo za asili, ninaomba mnipokee ngoma yangu inayokwenda kwa jina la kichomi ipo hewani na inapatiklana katika mitandao yangu yote ya kijamii.
“Nina uwezo wa kutunga na kuandika kama mtu atajitokeza kunisapoti tunaweza kukaa tukafanya kazi nina uhakika sito muangusha” amesema De Master
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED