Vyama vya michezo kitanzini

By Shufaa Lyimo , Nipashe
Published at 06:40 AM Aug 25 2024
Msajili wa vyama vya michezo, Evordy Kyando.
Picha: Mtandao
Msajili wa vyama vya michezo, Evordy Kyando.

VYAMA na mashirikisho ya michezo hapa nchini vimetakiwa kuwasilisha taarifa zao za fedha zilizopitiwa na wataalamu walioidhinishwa na Serikali kabla ya kufika Agosti 31 mwaka huu.

Hayo yalisemwa jana, na Msajili wa vyama vya michezo, Evordy Kyando wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo alivitaka vyama hivyo kuwasilisha taarifa zao za fedha za miaka miatano nyuma.

"Vyama na Mashirikisho ya Michezo vimetakiwa kuwasilisha taarifa  za matumizi ya fedha kwenye ofisi za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ambazo walizitumia kwa kipindi cha miaka mitano ya nyuma kwani tunataka kuzipitia taarifa hizo," alisema Kiando.

Aidha, alisema kwa muda mrefu vyama hivyo vimekuwa haviwasilishi taarifa zao na kusisitiza wale watakaoshindwa kuwasilisha taarifa zao watafutiwa uwanachama.

"Ninaomba viongozi wa vyama hivyo wawasisitize wanachama wao, wawasilishe taarifa zao ili kuepuka adhabu ya kufutwa uanachama," alisema. 

Alisema BMT imekuwa likizikagua taarifa hizo mara kwa mara ikiwa pamoja na  kuangalia rasilimali ya vyama vya michezo.