MNH-Mloganzila yaanza upandikizaji meno bandia kisasa

By Christina Mwakangale , Nipashe
Published at 08:37 PM Sep 12 2024
Wataalamu wa meno wakiendelea na upasuaji na upandikizaji meno kisasa.
PICHA: MNH-MLOGANZILA
Wataalamu wa meno wakiendelea na upasuaji na upandikizaji meno kisasa.

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH)-Mloganzila inaendelea imeanza upasuaji wa upandikizaji wa meno bandia kisasa.

Kambi ya siku tano kwa ajili ya huduma hiyo imeanza Septemba 10 hadi 14, mwaka huu kwa lengo la kuwahudumia wagonjwa 30.

Kambi hiyo inafanywa na wataalam wa ndani kwa kushirikiana na Daktari Bingwa aliyebobea katika upasuaji wa taya kutoka Hospitali za Wochhardt, Dk. Chirag Desai.
Upandikizaji huo utahusisha kupandikiza jino la mgonjwa moja kwa moja kwenye mfupa wa taya na kulifanya jino hilo kujishikiza na haliwezi kutoka kama yalivyo mengine ya bandia.

Mkuu wa Idara ya Kinywa na Meno kutoka Hospitali hiyo, Dk. Agrey Shao, amesrma mwitiko wa watu kupandikiza meno bandia umekuwa mkubwa, huku awali lengo likiwa kupandikiza wagonjwa 20, idadi imeongezeka hadi 30.