'Kuotea' kwa vunja mechi ya fainali FA Zanzibar

By Hawa Abdallah , Nipashe
Published at 06:09 AM Jun 16 2024
Mpira.
Picha: Mtandao
Mpira.

MCHEZO wa Fainali ya kombe la FA Zanzibar umelazimika kuvunjika katika muda wa ziada baada yadakika 90 baada ya mwamuzi kukataa goli la pili la JKU.

Mwamuzi wa mchezo huo, Mohamed Amour alilikataa bao hilo  kwa kuwa mfungaji alikuwa ameotea.

Mchezo huo wa fainali ulikuwa unachezwa kwenye uwanja wa Gombani, Pemba kati ya JKu dhidi ya wenyeji wao mChipukizi FC.

Mchezo huo ulilazimika kuongezwa dakika 30 za ziada baada ya dakika 90 kukamilika kwa timu zote kufungana bao 1-1.

Bingwa wa Michuano hiyo ataiwakikisha Zanzibar katika michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Africa.

Akizungumza na gazeti hili Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Soka visiwani hapa (ZFF), Suleiman Haji 'Kibabu', alisema sababu kubwa iliyopelekea  kuvunjika mchezo huo ni baada ya kukataliwa goli la JKU  katika dakika hizo za ziada na jambo lililopelekea kutokera vurugu zilisababisha mchezo huo kuvunjika.

Alisema baada ya kutokea vurugu hizo ambazo zilifanikiwa kutulizwa na maafisa usalama wa mchezo huo lakini cha kushangaza baada ya utulivu Mwamuzi aliamua kuuvunja mchezo huo.

“Bado hakukuwa na sababu ya msingi kwa maamuzi aliyoyachukua mwamuzi huyu pasipo kuwashirikisha waamuzi wenzake, licha ya kutokea vurugu lakini zilifanikiwa kutulizwa”alisema.

Hata hivyo alisema tayari washakutana na kufanya kikao juu ya mchezo huo na watatoa maamuzi kwa mujibu wa kanuni ya mashindano ya masimu wa 2023/2024.