Israel yaua Wapalestina 24 Gaza

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 05:15 PM Jun 25 2024
Moja ya vifaru vya jeshi vya Israel mjini Rafah.
Picha: Amir Levy/Getty Images
Moja ya vifaru vya jeshi vya Israel mjini Rafah.

MAAFISA wa Afya katika Ukanda wa Gaza, wamesema Jeshi la Israel limewauwa Wapalestina 24 katika mashambulizi matatu tofauti ya ndege mjini Gaza huku vifaru vikiingia ndani kabisa ya mji wa Rafah, kusini mwa Gaza.

Mashambulizi miwili kati ya hayo yalizilenga shule mbili katika mji wa Gaza na kusababisha vifo vya watu 14, na lingine lilishambulia nyumba moja eneo la Shati na kusababisha vifo vya watu 10.

Nyumba hiyo iliyoshambuliwa inamilikiwa na familia kiongozi wa Hamas, Ismail Haniyeh, ambaye anaishi Qatar, na shambulio hilo limemuuwa mmoja kati ya dada zake pamoja na ndugu wengine pia.

Haniyeh, ambaye anaongoza diplomasia ya Hamas na ndiye uso wa umma wa kundi hilo ambalo limekuwa likiongoza Gaza, amepoteza jamaa zake wengi katika mashambulizi ya anga ya Israel tangu Oktoba 7, wakiwemo wanawe watatu.