Waziri Mkuu aahirisha Shughuli za Bunge

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 03:58 PM Jun 28 2024
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Picha: Maktaba
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

SHUGHULI za Bunge zimeahirishwa hadi Agosti 27, 2024, baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutoa hoja ya kuahirisha kisha hoja kuungwa mkono na wabunge.

Waziri Mkuu ametoa hoja hiyo leo Juni 28, 2024 baada ya mkutano wa 15 wa Bunge la 12 kumaliza shughuli zake zilizopangwa kwa muda wa miezi mitatu ambapo ilikuwa ni kupokea, kujadili na kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2024/2025.