Daktari Bingwa wa Magonjwa ya ndani, Meja Godfrey Mutafungwa, amewataka watanzania kuzingatia lishe bora na kujiepusha na ulaji wa chumvi, sukari na mafuta mengi ili kujiepusha na magonjwa mengi ya ndani na yasiyo ya kuambukiza.
Meja Dk. Mutafungwa alitoa ushauri huo leo akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa huduma za matibabu kwenye kambi maalum inayoendelea jijini Arusha.
Amesema wengi aliowahudumiwa walikuwa wakiishi bila kutambua kama wana matatizo ya shinikizo la damu na kisukari.
Aidha, amewataka wananchi kuwa na utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara ili kubaini ikiwa wana maambukizi au matatatizo ya afya kuanza matibabu kabla ya kuathirika zaidi.
Amesema watanzania wanatakiwa kuzingatia na kufuata maelekezo ya madaktari na kuacha kutumia dawa mbalimbali ikiwemo za kienyeji bila ya kupima.
Dk. Mutafungwa amewashauri wananchi kuzingatia kufanya mazoezi mara kwa mara kwa kuwa tafiti zinaonesha kuwa kutoka jasho ama kufanya mazoezi kunaepusha watu na magonjwa mbalimbali hasa yasiyokuwa ya kuambukiza.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED