Zawadi za washindi wa NMB Pesa zawafikia mtaani kwao

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 06:12 PM Jun 25 2024
Zawadi za washindi wa NMB Pesa zawafikia mtaani kwao.
Picha: Mpigapicha Wetu
Zawadi za washindi wa NMB Pesa zawafikia mtaani kwao.

WASHINDI wa Kampeni ya Weka, Tumia na Ushinde Kutoka Benki ya NMB, jana walikabidhiwa zawadi huku umati mkubwa wa wakazi wa Dodoma ukishuhudia tukio hilo.

Kutolewa kwa zawadi hizo ni hitimisho la Kampeni hiyo ya miezi mitatu iliyofikia mwisho wake Mei mwaka huu ambapo zawadi mbalimbali zenye thamani ya zaidi ya Sh250 Milioni zimeshakabidhiwa kwa washindi.

Akikabidhi zawadi kwa washindi, Mkuu wa Idara ya mauzo na mtandao wa Matawi wa Benki ya NMB, Donatus Richard alisema Kampeni hiyo ilianza rasmi mwezi Machi mwaka huu na ilipofika mwisho mwa mwezi Mei walitangaza washindi waliofikia 126.

Richard alisema mshindi wa jumla ni aliyepata Sh 10 milioni ambaye alitangazwa Emmanuel Amos Kakale mkazi wa wilaya ya Ikundi mkoani Singida huku wengine wakiibuka na pikipiki za miguu mitatu 8, friji, pesa taslimu, majiko ya gesi na TV.

`1
Meneja huyo alisema lengo la akaunti hiyo ni kuwapa nafasi Watanzania kuingia kwenye mfumo wa kipesa ikiwemo wafanyabiashara ndogondogo na wakulima ambao walikuwa wanashindwa kwenye masharti ya ufunguaji akaunti na mikopo.

Tulikuwa na aina tofauti za kuwapata washindi, kwa mfano kulikuwa na droo ya wiki ambayo washindi 10 kila mmoja alipata 500,000 na kwa wiki tisa mfululizo tulikuwa na washindi 90, kulikuwa na washindi watano wa kila mwezi hivyo tulipata washindi 10 ambapo kila mmoja alinyakua Sh 10 milioni lakini kulikuwa na matamasha ya kutoa zawadi mbalimbali,” alisema Richard.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Hundi ya Sh 10 Milioni Emmanuel Kakale alisema mbali na kupewa mfano wa Hundi kwa jana, lakini muamala wa fedha ulishatumwa kwenye akauti yake na alishathibitisha kuzipokea.

Kakale alisema kilichompa ushindi ni namna alivyokuwa akitumia fedha hizo licha ya kuwa hakuwa amelenga kwenye shindano bali ni utaratibu wake kutumia NMB kwenye miamala mbalimbali ikiwemo malipo na ununuzi wa bidhaa.

2

Hata hivyo alikiri kwamba ilikuwa ni ngumu kuamini kama ameshinda hasa alipopigiwa simu na maofisa kutoka NMB hadi alipoona fedha imeingia kwenye akaunti yake ndani ya benki hiyo.

Awali Meneja wa NMB Kanda ya Kati Janeth Shango alisema mbali na zawadi walizopata washindi hao, lakini kuna faida nyingi kwa watumiaji wa akaunti za NMB ikiwemo mikopo ya Mshiko Fasta inayoanzia na Sh 1000 hadi Sh 1 Milioni.

Shango aliwaomba Watanzania kuendelea kuitumia NMB katika kuweka na kutunza fedha zao kwani ni benki yenye matawi hadi maeneo ya vijijini ambayo inaweza kuwapa huduma bila kuwa na usumbufu.

3

Mbali na zawadi ya mshindi wa fedha taslimu, NMB imekabidhi TV janja, jokofu la milango miwili, jiko la gesi, pikipiki 4 za magurudumu matatu na zawadi zingine zilipelekwa katika mikoa ambayo washindi walitokea.

Miongoni mwa waliopokea na zawadi zao kwenye mabano ni Emmanuel Kakale (Sh 10 Milioni), Dickson Nchimbi (Friji la milango miwili), Rusia Mathias (Jiko la gesi), Michael Tilya (TV Kubwa) na Agnes Kipalile, Catherine Amori, Denis Thionest na Ramadhan Msigati waliopata pikipiki za miguu mitatu.

4