SPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika bonanza la Bunge litakalofanyika kesho kwa kushirikisha mashabiki wa timu za Simba na Yanga, jijini hapa.
Bonanza hilo lenye kauli mbiu ‘Utani wetu, Umoja wetu’ litahudhuriwa pia na viongozi, wanachama na mashabiki wa timu hizo kongwe nchini.
Akizungumza jijini hapa jana, Mwenyekiti wa bonanza, Festo Sanga, alisema pia watakuwa na mgeni maalum ambaye ni Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia huku na mwamuzi mstaafu wa FIFA, Othman Kazi.
Sanga alisema bonanza hilo litatumika kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi kwa wingi kutokana na tishio kubwa la magonjwa yasiyoambukiza.
Aidha, alisema bonanza lengo lake ni kuleta mahusiano ya pamoja na taasisi mbalimbali zilizoko Dodoma zitashiriki ambazo zina mashabiki wa Simba na Yanga.
Meneja wa Benki ya Azania wa Tawi la Dodoma, ambao ndio wadhamini wakuu wa bonanza hilo, Liberia Peter, alisema michezo hiyo imeandaliwa kwa ajili ya kuhamasisha na kuimarisha afya za Watanzania.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED