RAIS Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya miaka 48 ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambayo yatafanyika Kitaifa jijini Dodoma Februari 5, mwaka huu.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama hicho Taifa, Fadhili Maganya, alisema hayo jana jijini hapa, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhalizi ya maadhimisho hayo kitaifa.
“Chama kitakuwa kinaadhimisha miaka 48 ya kuzaliwa kwake, sisi Jumuiya ya Wazazi ya CCM tumepewa jukumu la kuanza chereko chereko za sherehe hizi ambazo kilele ni Februari 5, mwaka huu hapa Dodoma,”alisema
Alisema, katika maadhimisho ya mwaka huu yataambatana na shughuli mbalimbali ikiwemo kongamano litakalofanyika Frebruari 2, mwaka huu ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete ambalo utakutanisha watu 3,500.
“Tutakua na kongamano ambalo limelenga kuleta watoa mada mbalimbali wasomi, viongozi, makada, na wanajamii ambao watazungumzia mahali ambapo chama kimetoka, kilipo na kinapokwenda,”alisema
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED