Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Steven Wasira, amewakosoa wanaoshinikiza upatikanaji wa Katiba Mpya huku wakipuuzia masuala ya maendeleo. Akizungumza mjini Bunda, Januari 30, 2024, Wasira alihoji iwapo Katiba mpya ndiyo suluhisho la changamoto zinazowakabili Watanzania.
"Wanalilia Katiba Mpya lakini hawafikirii wananchi. Watanzania wanahitaji maji, shule, barabara, huduma bora za afya na mambo mengine ya maendeleo. Wao wameshikilia Katiba Mpya, je, watu watakula Katiba?" alihoji Wasira.
Katika hotuba yake kwa wanachama wa CCM, Wasira alisisitiza kuwa chama hicho hakina mpango wa kuondoka madarakani, akipuuza madai ya wapinzani wanaodai kuwa muda wa CCM umekwisha.
"Mtu mzima mwenye akili timamu anauliza eti CCM itaondoka lini madarakani? CCM haiondoki, Ng’o!" alisema kwa msisitizo.
Ziara ya Wasira inakuja siku chache baada ya kuteuliwa na kupitishwa kushika nafasi hiyo ya uongozi ndani ya CCM.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED