Bukombe Runnings Club zafana Geita

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 02:28 PM Oct 10 2024
Bukombe Runnings Club zafana Geita
Picha: Mpigapicha Wetu
Bukombe Runnings Club zafana Geita

Naibu Waziri Mkuu Dotto Biteko amewaongoza wananchi na watumishi wa serikali wilayani Bukombe kwenye mbio za Bukombe Runnings club zilizofanyika leo Oktoba 10,2024 kwa kukimbia umbali wa kilometa 3.3.

Mbio hizo zimeanza kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya wa Geita na kuhitimishwa kwenye uwanja wa Kilimahewa wilayani humo. 

Mbio hizo za Bukombe runnings club zimefanyika ikiwa ni siku moja kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya mwalimu, ambayo inatarajiwa kuhitimishwa  kesho kwenye mji mdogo wa  Ushirombo.

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Paskasi Muragili akizungumza baada ya washiriki kuhitimisha mbio hizo amewataka wananchi kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi kwakuwa mbali na michezo kuchangamsha mwili pia ni afya.

Maadhimisho ya siku ya mwalimu duniani kwa wilaya ya Bukombe inatarajiwa kufanyika kesho  Oktoba11,2024 na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.