Ijue Miaka 60 ya ubia China - Tanzania, na karata aliyotumia Dk. Samia Beijing

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 09:12 AM Sep 13 2024
Rais Samia Suluhu Hassan, alipokuwa kwenye mazungumzo na Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema katika ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa nchini Ethiopia, mwaka jana.
PICHA: MTANDAO.
Rais Samia Suluhu Hassan, alipokuwa kwenye mazungumzo na Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema katika ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa nchini Ethiopia, mwaka jana.

HADI sasa si nchini au Afrika pekee, ni hadi kimataifa, gumzo lililotawala ni Mkutano wa Tisa uliofanyikia jijini Beijing, baina ya Afrika na China, Rais Xi Jinping, akiwa mwenyeji wao.

Kikubwa ndani yake, kimetawala yaliyoamuliwa na kutangazwa rasmi na China, uwekezaji wa China Dola za Marekani Bilioni 51, ikiangaza kukopesha nchi za Kiafrika kwa maendeleo hasa ya miundombinu, vilevile haikukaa mbali a na ushirikiano wale wa kihistoria, kwamba iko tayari kutoa msaada wa kijeshi, ikitaja kiwango maalum cha fedha. 

China inahitaji nini? Hapo ikaweka wazi kwamba inachotarajia kutoka Afrika ni soko la bidhaa zake. Hivyo kuna ‘nipe nikupe,’ ikizingatiwa baada ya kuvunja Dola Kuu la Mashariki Duniani (Warsaw Pact) dhidi ya Magharibi, China ikajipanga tena kiuchumi na sasa ni taifa linalotisha kiuwezo katika ulimwengu wa soko, hata kuinyima usingizi Marekani na mshirika wake, nchi za Jumuiya ya Ulaya (EU). 

Ni hoja iliyozua mjadala wa kidunia, kwamba uamuzi huo wa China una maana gani, ingawaje hatua kama hiyo ilishachukuliwa na Marekani, pia Russia, kuingia makubaliano ya kibiashara. 

Lakini katika namna ya kipekee, Tanzania na jirani yake Zambia zimeonekana kuwa zimetupa karata zao mapema, wakiwa katika hatua ya kutiwa saini makubaliano ya awali ikihusu ukarabati wa reli yao ya TAZARA, ambayo imeharibika na haiko katika ufanisi. 

Ni reli iliyojengwa kati ya mwaka 1970 na 1975, kwa mkopo usio na riba kutoka China.  Hilo linafanya kwa anayehoji kulikoni Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na Haiakinde Hichilema, wamevuka vipi kuifika hatua hiyo. 

Pia, mkuu huyo wa Zambia, naye akatikisa kwa nafasi yake, kwa makubalino kama hayo huko Beijing, kukaundwa mradi wa umeme nchini kwake kwa msada wa China. 

TANZANIA NA CHINA 

Mzizi wa Tanzania na China kuingia uhusiano rasmi ni mwaka 1964, nchini kulipofanyika uamuzi mkuu wenye sura nne; Mosi, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kuunda Tanzania; taifa kuingia katika muundo wa kisiasa na utawala hodi, siasa ya chama kimoja. 

Pia, ni mwaka ilipoundwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ikichukua nafasi ya awali iliyoanza nayo kutoka uhuru wa nchi, historia ambayo imeshaelezwa kwa kiasi kikubwa katika maadhimisho ya miaka 60 ya jeshi hilo yanayoendelea. 

Mwisho, ni kuundwa kwa Mpango wa Kwanza wa Miaka Mitano wa Maendeleo ya Nchi (1964- 1969), ambao hasa ulitafsiri namna nchi inajipanga hasa kwa upande wa Bara na ukaendelezwa kwa miaka iliyofuata. 

Ni mpango ambao unabeba sura kamili ya kinachopaswa kufanywa na Tanzania kwa miaka yote tangu wakati huo, ukiwa mfano wa katiba kuu, mipango inaangukia mstari huo hadi sasa. 

Katika hatua hiyo ya kwanza mwaka 1964, Tanzania ilikuwa haijajitoshesheleza kwa mengi na kiuchumi nchini na wananchi wake waliokuwa wanatumia wasichokizalisha na kuazalisha wasichokitumia. 

Mapengo yalikuwa dhahiri katika sekta zote, elimu fursa zake zilikuwa chache na walioelimika na wataalamu walihesabika na mapengo kama hayo katika sekta muhimu kama za kilimo, afya, biashara na viwanda. 

Hapo maana yake serikali ya Tanzania ilipaswa kuwezaje kwa kina katika kujitosheleza kufanikisha hilo, huku uwezo wa kiuchumi nchini ulikuwa chini sana, maana ni miaka mitatu tu tangu kupatikana uhuru. 

Moja ya mataifa rafiki ambayo hata katika sera za kisiasa ziliendana na nchi ilikuwa China na kwa maana hiyo, Rais Mao Tse Tung a Mwalimu Julius Nyerere, wakaanza kufanyia kazi. 

Moja ya mazao yake ya awali katika hilo, ni kutoa usaidizi kwa staili ya kujengea uwezo nchi, ikiwamo katika sekta kama Ulinzi na Usalama na ikizingatiwa katika upande wa pili wa shilingi, hali za ukoloni mamboleo na mapinduzi Afrika, yalikuwa juu sana wakati huo, nchi nyingi zikitoka kupata uhuru. 

Mwaka 1967, serikali ikiwa inatekeleza Mpango wa Kwanza wa Maendeleo na kukafanyika Azimio la Arusha, iliyoweka miradi yote kitaifa katika himaya ya serikali. Mwaka mmoja baadaye, kupitia mazungumzo binafsi ya marais Mao Tse Tung, Kenneth Kaunda na Mwalimu Nyerere, upakatikana mradi wa TAZARA. 

Nyerere na Kaunda wakiwa waumini wa itikadi moja, chini ya Umoja wa Nchi Huru za Afrika, wakaingia katika mradi huo wa TAZARA mwaka 1970 ambao ni wa kiuchumi, pia upande wa pili siasa, ukikwepa matumizi ya bandari za Msumbiji kuliokuwa koloni la Ureno, pia utawala wa makaburu wa Afrika Kusini. 

Miaka yote baada ya hapo, China imedumu kuiwa mshirika wa Tanzania, ikijidhhirisha katika matendo ya kihistoria, kundi kubwa la Watazanania hadi miaka ya 1980 wakarejea kutoka USSR na China na madakatari wengi wa Hospitali ya Ocean Road  na Muhimbili, Dar es Salama wakiwa wahitikimu wa nchini hizo, huku USSR ikiwa na chuo kikuu malaum kwa Waafrika – Lumumba.  

Kwa maana hiyo, ndani ya uhusiano wa kudumu wa Tanzania na China, mradi mpya wa Hichlime na Dk. Samia, wametumia kuwa karata yao ya maendeleo, hata kupatikana mradi huo wa TAZARA, wakijinadi nao mapema hata kabla ya mkutano wa Bejing wiki iliyopita. 

Katika sura nyingine imekuwa mradi wake maalaum Rais Dk. Samia katika mikakati mipyo yake kimaendeleo ambayo nchi inayo katika uhusiano na China. 

Sura nyingine ya uhusiano katika siasa, inajionyesha hata katika ziara mahsusi ya Rais Xi Jinping, wastani wa miaka tisa iliyopita, akiwa na kundi kubwa la wafanyabiashara waliofika. 

Pia, katika  ziara za awali ugenini, Katibu Mkuu wa CCM  Daniel Chongolo, katika ziara za awali akaifanya nchini China, kama alivyofanya Rais Samia, ikiasharia uwekezaji wake huko. Majumuisho ya yote inaanika ishara ya ubia wa Tanzania, Zambia kwa Wachina.