Mradi wa Maji Kigonsera Mbinga Vijijini kuongeza upatikanaji maji

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 05:51 PM Sep 25 2024
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso.

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema Serikali inatekeleza jumla ya miradi nane ya maji katika Jimbo la Mbinga Vijijini sambamba na iliokamilika kufikia jumla ya Miradi 14 ya kiasi cha Bilion 13.9 ambapo kukamilika kwa miradi yote kutapelekea upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama kufikia zaidi ya asilimia 86.7.

Waziri Aweso ameyasema hayo leo Septemba 25 ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan wakati aliposimama na kusalimiana na wananchi wa Jimbo la  Mbinga Vijijini Mkoani Ruvuma.

Aidha Amewahakikishia wakazi wa Kigonsera ambayo ni makao makuu ya halmashauri ya Mbinga vijijini kwamba kutokana na ongezeko kubwa la watu na kukua kwa mji serikali ipo hatua ya kumpata mkandarasi atakae jenga Mradi wa kiashi cha shilingi Bilion 9 na kazi inatarajiwa kuanza mwezi novemba.