Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amewahimiza wananchi kujisajili katika mfumo wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), ili kunufaika kikamilifu na huduma mbalimbali zinazotolewa kupitia mifumo iliyounganishwa.
Katambi amesema usajili wa NIDA ni hatua muhimu inayowezesha wananchi kuepuka usumbufu, kwa kutambuliwa kwa urahisi na kupata huduma kwa haraka katika taasisi mbalimbali za umma na binafsi.
“Kitambulisho cha Taifa kinarahisisha upatikanaji wa huduma nyingi muhimu kwa jamii, ikiwamo hospitali, vyuo, umeme, maji, benki, hati za kusafiria, leseni za magari na biashara, utambulisho wa mlipa kodi (TIN),
Usajili wa kampuni binafsi, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (mafao ya uzeeni au fidia kazini) na nyingine nyingi. NIDA inaondoa vikwazo kwa wananchi wanapohitaji huduma za msingi,” amesema.
Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, James Kaji, amesema zinashughulikia changamoto za majina kwa wananchi wenye sababu na vielelezo stahiki linaendelea, ikiwamo kwa wale waliopata msamaha wa Rais kuruhusiwa kurekebisha taarifa zao za NIDA.
Aliwahimiza wananchi ambao bado hawajachukua vitambulisho vyao katika ofisi za NIDA za wilaya kwenda kuvichukua, ili waanze kunufaika na matumizi yake katika kupata huduma mbalimbali.
© 2026 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED