Zaidi ya vikundi 100 vya wanawake kutoka Mkoa wa Dar es Salaam vitapata mafunzo ya uwezeshwaji kiuchumi, ili kuongeza tija uelewa na ubunifu katika shughuli zao.
Mbunge wa Viti Maalum kutoka Mkoa wa Dar es Salaam, ambae pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Amo, Amina Said, amesema mafunzo yatawalenga makundi yote ya wanawake yanayofanya shughuli za kiuchumi, ili waweze kujiongezea kipato.
Mafunzo hayo yanatarajiwa kufunguliwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Halima Mamuya.
© 2026 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED