Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu wanne akiwamo mwanachuo mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Iringa, Lenad Shamba (21), mkazi wa Tarime Mkoa wa Mara wamekamatwa wakisafirish dawa za kulevya.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, SACP Benjamin Kuzaga, aliwataja watuhumiwa wengine kuwa ni James Mwakalebela (26), mkazi wa Ngonga Kyela na Joseph Mkwara (26) na Wilfred Komba (24), walikutwa wakisafiri dawa hizo aina ya bhangi yenye uzito wa kilo 45 na gramu 785 katika nyakati tofauti.
Kamanda amesema watuhumiwa walikamatwa wakiwa na dawa hizo za kulevya zikiwa kwenye mabegi matatu na mifuko miwili ya sandarusi wakizisafirisha kwa mabasi ya abiria kutoka Mbeya kuelekea Dar es Salaam.
Amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa waliingiza dawa hizo nchini kutokea nchi jirani.
© 2026 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED