Baada ya kukaa mahabusu gerezani kwa siku 88, viongozi wa CHADEMA mkoani Kigoma, akiwemo Mwenyekiti wa Mkoa Rajabu Mfaume Bujoro na Mwenyekiti wa Wilaya ya Kasulu Phanuel Eliabi Kisabo, pamoja na wenzao watatu, wameachiwa huru leo Februari 10, 2026.
Viongozi hao wameachiwa na Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Kigoma baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuwasilisha taarifa ya kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi dhidi yao.
Katika shauri hilo, viongozi hao walikuwa wakitetea na Wakili Dickson Lucas Matata, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Magharibi.
© 2026 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED